Posts

137. YESU MPONYA

YESU MPONYA 1.   Yesu ndiye mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira. Chorus: Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge. 2.   Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo. 3.   Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani. 4.   Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta. 5.   Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya.

138. TUKUTENDEREZA YESU (LUGANDA)

TUKUTENDEREZA YESU (LUGANDA) 1.   Yesu, Mulokozi wange: Lero nze wuwo wenka; Omusaigwo gunazi’za Yesu Mwana gwendiga. Chorus: Tukutendereza, Yesu, Yesu Mwana gwendiga; Omusaigwo gunazi’za; Nkwebaza, Mulokozi. 2.   Eda nafuba bufubi Okufuna, emirembe; Lero maliride dala Okweyabiza Yesu. 3.   Nababuliranga bantu Obulokozi bwona, Obutali bwa kitundu Obulamba obwobuwa. 4.   Nategezanga ebya Yesu Nobuvumunesitya; Eyanziya mu busibe Nokuwonya eyamponya. 5.   Nebaza eyanunula nze; Eyamponya wa kisa! Yesu ankuma Ansanyusaera, Bulijo yebazibwe.

139. NURU YA ROHONI

NURU YA ROHONI   1.    Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu. Nakuomba sana niangazishe; ukanitazame kwa huruma tu, ukanitulize mimi maskini. 2.   Futa dhambi zangu kwa damu yako. Hasira ya Mungu iniondoke. Machubuko yako, hata mateso, niyawaze vema rohoni mwangu. 3.   Nakutumaini peke yako tu, niwe mtumwa wako pote nilipo utanikubali sina mashaka! Nitakushukuru pasipo mwisho.

140. MAHALI NI PAZURI

MAHALI NI PAZURI 1.    Mahali ni pazuri, ndugu wanapokaa, wakipatana vema, na wakipendana. 2.    Kama umande mzuri, unyweshavyo shamba, vivyo na Mungu wetu, hubariki ndugu. 3.   Upendano hujenga, boma zuri kwao, wakae na amani, waliookakoka.  4.   Na ulimwengu wote, watiwa nuruni, halafu kundi moja, na mchunga mmoja tu.

141. PANA JITO, LINA MAJI MAZURI

PANA JITO, LINA MAJI MAZURI 1.    Pana jito, lina maji Mazuri, Yaenda ulimwenguni. Lametameta nalo Linang’aa. Walijua jito hilo? Chorus: Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe. 2.   Wanywao maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa. Makosa na shida Yanaondoshwa, Wote waoshwa na Bwana. Ninakuita nawe njoo… 3.   Jito hilo latoa maji mengi, matamu yapendezayo. Yaponya wagonjwa, Yatia nguvu, Uchafu watakashika. Ninakuita nawe njoo… 4.   Maji ya jito hilo ni uzima unaotoka Kwa Yesu. Damu yake yenye kiasi kikuu Imemwagwa tusafike. Ninakuita nawe njoo…

142. BABANGU KULE MBINGUNI

BABANGU KULE MBINGUNI 1.    Babangu kule mbinguni, aliye juu pa malaika, aangalia njia zangu na kunilinda maisha. 2.    Hata unywele kichwani hauanguki ovyo tu na siri zote za moyoni zajulikana kwa Baba. 3.   Zamani nisipojua, amekwisha kuandika mkononi mwake jina langu, ndio upedo wake mkuu. 4.   Ee Baba yangu u mwema, nami nataka kufanya kama malaika wafanyavyo mbinguni kwako milele!

143. NCHI NZURI YAMETAMETA

NCHI NZURI YAMETAMETA 1.   Nchi nzuri yametameta, Huonekana kule mbali, Naye Yesu hutuongoza. Tukafike na sisi huko. Chorus: Sisi mbali, karibu, Tutaimba na sisi huko! 2.   Kule tutawaona wengi Wapendwao na Yesu Bwana, Tutashirikiana nao Itakuwa furaha kubwa. Si mbali.. 3.   Tutamwona na Bwana Wetu, Yesu kristo mwokozi Wetu, Tutashangilia daima, Tuna hamu ya kwenda Kwetu. Si mbali..