Posts

Showing posts from March, 2022

137. YESU MPONYA

YESU MPONYA 1.   Yesu ndiye mganga wetu Aponya wagonjwa wote; Mganga wetu ni Yesu, Aponyaye hasira. Chorus: Tumsifu huyo Yesu Tumsifu milele, Kwani Mponya mtakata Mwokozi wa wanyonge. 2.   Mganga wetu ni Yesu Huondoa matusi; Mganga wetu ni Yesu, Mwenye kuponya choyo. 3.   Mganga wetu ni Yesu Huponya wivu wetu; Yesu ndiye aponyae Kelele za nyumbani. 4.   Mganga wetu ni Yesu Mponya wa tamaa mbaya; Mganga wetu ni Yesu Uasherati hufuta. 5.   Mganga wetu ni Yesu Aponya kiu cha pombe, Mganga wetu ni Yesu Kila dhambi uponya.

138. TUKUTENDEREZA YESU (LUGANDA)

TUKUTENDEREZA YESU (LUGANDA) 1.   Yesu, Mulokozi wange: Lero nze wuwo wenka; Omusaigwo gunazi’za Yesu Mwana gwendiga. Chorus: Tukutendereza, Yesu, Yesu Mwana gwendiga; Omusaigwo gunazi’za; Nkwebaza, Mulokozi. 2.   Eda nafuba bufubi Okufuna, emirembe; Lero maliride dala Okweyabiza Yesu. 3.   Nababuliranga bantu Obulokozi bwona, Obutali bwa kitundu Obulamba obwobuwa. 4.   Nategezanga ebya Yesu Nobuvumunesitya; Eyanziya mu busibe Nokuwonya eyamponya. 5.   Nebaza eyanunula nze; Eyamponya wa kisa! Yesu ankuma Ansanyusaera, Bulijo yebazibwe.

139. NURU YA ROHONI

NURU YA ROHONI   1.    Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu. Nakuomba sana niangazishe; ukanitazame kwa huruma tu, ukanitulize mimi maskini. 2.   Futa dhambi zangu kwa damu yako. Hasira ya Mungu iniondoke. Machubuko yako, hata mateso, niyawaze vema rohoni mwangu. 3.   Nakutumaini peke yako tu, niwe mtumwa wako pote nilipo utanikubali sina mashaka! Nitakushukuru pasipo mwisho.

140. MAHALI NI PAZURI

MAHALI NI PAZURI 1.    Mahali ni pazuri, ndugu wanapokaa, wakipatana vema, na wakipendana. 2.    Kama umande mzuri, unyweshavyo shamba, vivyo na Mungu wetu, hubariki ndugu. 3.   Upendano hujenga, boma zuri kwao, wakae na amani, waliookakoka.  4.   Na ulimwengu wote, watiwa nuruni, halafu kundi moja, na mchunga mmoja tu.

141. PANA JITO, LINA MAJI MAZURI

PANA JITO, LINA MAJI MAZURI 1.    Pana jito, lina maji Mazuri, Yaenda ulimwenguni. Lametameta nalo Linang’aa. Walijua jito hilo? Chorus: Ninakuita nawe njoo! Utafute jito hilo! Maji yake yapoza Moyo. Nawe yateke unywe. 2.   Wanywao maji haya wafurahi, waimba kwa shangwe kubwa. Makosa na shida Yanaondoshwa, Wote waoshwa na Bwana. Ninakuita nawe njoo… 3.   Jito hilo latoa maji mengi, matamu yapendezayo. Yaponya wagonjwa, Yatia nguvu, Uchafu watakashika. Ninakuita nawe njoo… 4.   Maji ya jito hilo ni uzima unaotoka Kwa Yesu. Damu yake yenye kiasi kikuu Imemwagwa tusafike. Ninakuita nawe njoo…

142. BABANGU KULE MBINGUNI

BABANGU KULE MBINGUNI 1.    Babangu kule mbinguni, aliye juu pa malaika, aangalia njia zangu na kunilinda maisha. 2.    Hata unywele kichwani hauanguki ovyo tu na siri zote za moyoni zajulikana kwa Baba. 3.   Zamani nisipojua, amekwisha kuandika mkononi mwake jina langu, ndio upedo wake mkuu. 4.   Ee Baba yangu u mwema, nami nataka kufanya kama malaika wafanyavyo mbinguni kwako milele!

143. NCHI NZURI YAMETAMETA

NCHI NZURI YAMETAMETA 1.   Nchi nzuri yametameta, Huonekana kule mbali, Naye Yesu hutuongoza. Tukafike na sisi huko. Chorus: Sisi mbali, karibu, Tutaimba na sisi huko! 2.   Kule tutawaona wengi Wapendwao na Yesu Bwana, Tutashirikiana nao Itakuwa furaha kubwa. Si mbali.. 3.   Tutamwona na Bwana Wetu, Yesu kristo mwokozi Wetu, Tutashangilia daima, Tuna hamu ya kwenda Kwetu. Si mbali..

144. MBELE NINAENDELEA

MBELE NINAENDELEA 1.    Mbele ninaendelea, ninazidi kutembea. Maombi uyasikie, Ee Bwana, unipandishe. Chorus: Ee, Bwana, uniinue, Kwa imani nisimame; Nipande milima yote, Ee Bwana, Unipandishe. 2.   Sina tamani nikae, Mahali pa shaka, kamwe; Hapo wengi wanakaa, Kuendelea naomba. 3.   Nisikae duniani, asumbuapo Shetani; Natazamia mbinguni, nitafika na imani. 4.   Nataka nipandishwe juu, Zaidi yale mawingu. Nitaomba nifikishwe, Ee Bwana unipandishe.

145. NDOA YETU NZIMA

NDOA YETU NZIMA 1.   Ndoa yetu nzima simika, Yesu! Usiku na mchana uwepo kwetu. Leo tuna raha, Wewe watupa. Chorus: Ndoa yetu Bwana ndiwe Baraka! 2.   Atoka kijana, ataka mhumba siku zinapita za kupimana. Leo twapatana pamoja kukaa. Ndoa yetu... 3.    Vyote hapa chini vinakaa muda, vyote vinaoza, tena vyachakaa. Pendo la duniani nalo huchakaa. Ndoa yetu… 4.    Kakaa kwetu Bwana, kutukagua, pendo letu sisi lisichakae: Hivi na tukae na baraka tu. Ndoa yetu… 5.    Kana arusuni ulialikwa, walivyoishiwa ukaongeza, nasi shida zetu utazishinda. Ndoa yetu...

146. NENO LA MUNGU TAKATA

NENO LA MUNGU TAKATA 1.    Neno la Mungu takata Lililotoka mbinguni; Ambalo moto na panga Haziwezi kulishinda. Chorus: /: Twakushika siku zote Maishani na kufani. :/ 2.   Waliotutangulia Waliokutegemea, Wamekufia mashujaa; Nasi tulio watoto. Twakushika… 3.   Neno la Mungu takata, Tukushuhudie nasi Kwa neno tamu na tendo Kunako wenzi au adui. Twakushika…

147. TEGEMEA HADI KUFA

TEGEMEA HADI KUFA 1.    Tegemea mpaka kufa, Utapata wokovu. Bwana Yesu ni Mwokozi Yeye anakupenda. Uje kwake ‘sikawie’. Yeye akuokoa. Chorus: Njoo upesi! Njoo upesi! Fika kwa Bwana Yesu. 2.   Acha mambo ya dunia Yakuhangaishayo. Iko mali ya uzima Unaitiwaa hiyo. Mali hiyo ni uzima Utapewa na Bwana. Njoo upesi! … 3.   Wakatae, waepuke Wanaokudanganya; Na wajinga, wakuponza, Wakupoteza wewe. Ila wewe ukatae Kuondoka kwa Yesu. Njoo upesi! … 4.   Ukijua jambo hilo Usipolifuata Kosa hilo kubwa sana, Wapasiwa hukumu. Vumilia, jizuie Utapata uzima. Njoo upesi! … 5.   Bwana Yesu amekwisha Kukutengenezea Kitu chema kwake Mungu, Ndiko unakokwenda. Kile kitu upendacho Kule utakipewa. Njoo upesi! …

148. ONDOKENI! TUNAITWA

ONDOKENI! TUNAITWA 1.    Ondokeni! tunaitwa na walinzi wa juu mnarani Yerusalemu, amka wee! Ni usiku wa manane, yuaja Bwana wa arusi, wanawali wako wapi? Amkeni upesi! Kaziwasheni taa. Haleluya! Fuateni arusini kwenda kumpokea Bwana! 2.   Sayuni anasikia, moyo waruka kwa furaha, yu macho anaondoka. Mponya wake anashuka mbinguni mwenye utukufu, aleta mwanga wa kweli, taji yake yaja na Mwana wa Mungu. Hosiana! Twafuata kwenye shangwe tukale karamu yake. 3.   Waimbiwa nyimbo nzuri kwa misemo ya watu wote na ya malaika mbinguni. Tukifika mjini kwako kwenye milango ya malulu tutakuimbia nasi. Furaha kama hii haijasikiwa duniani. Nasi sasa tunaimba, tunakusifu, Ee Bwana.

149. HAYA, UMATI WA YESU

HAYA, UMATI WA YESU 1.    Haya, umati wa Yesu, Ulioungwa naye! Haya, enendeni hima Katika vita kubwa! Shetani tayari, Kupigana na sisi! 2.   Tumfuate Yesu Kristo, Tumwamini yeye tu. Mwovu akituvizia Sisi hatuogopi. Majeshi ya mbingu Ni pamoja na sisi! 3.   Tukikesha na kuomba Yesu anayotaka, Tukishika neno lake Na kumtegemea. Kwa nguvu hizi tu Tutaweza kushinda! 4.   Sasa haya wenzi wangu, Tumfuate Yesu tu! Siku za maisha yetu, Tuwe katika yeye. Tuache dunia Kuingia mbinguni! 5.   Pale Mungu atawapa Taji walioshinda, Wapate urithi wao Nyumbani mwa milele. Hayani! Tuimbe, Tumsifu Bwana wetu!

150. HAYA, EE MOYO WANGU

HAYA, EE MOYO WANGU 1.   Haya ee moyo wangu, imba kwa furaha. Umwimbie Muumbaji mbingu na dunia. Atukuzwaye pote umsifu na wewe kwa nguvu zako zote, umri wako wote. 2.   Mungu wake Yakobo. ndiye Mungu wwetu. Ukimchagua yeye, una fungu jema, unacho kitu chema, umepata mali; moyo utakung’aa shida zitakwisha. 3.   Ni mwenye nguvu nyingi, hana amshindaye, kwa hekima aumba vyote ni ajabu, misitu na mabonde, milima,mashamba, vilivyo baharini wanyama porini. 4.   Ana mizungu mingi, kuponya wanawe. Anawapa riziki, hata siku za njaa. Wenye chakula haba wanenepa miili: hata waliofungwa anawafungua. 5.   Mashangilio yote hayamtoshi yeye. Ni mwema peke yake nami ni vumbi tu! Ananihurumia kwa kuwa ni wake, kwa hiyo nalikuza Jina lake pote.

151. USIKU MTAKATIFU

USIKU MTAKATIFU 1.    Usiku mtakatifu! Wengine walala Wakeshao ni Yosefu tu na Maria waliomlinda Yesu mwana mzuri Yesu mwana mzuri. 2.   Usiku mtakatifu! Wachunga wapewa habari nzuri na malaika, zienezwe popote sasa: Yesu Mponya kaja Yesu Mponya kaja. 3.   Usiku mtakatifu! Siku ya furaha imetuangaza Kimungu tumepewa ukombozi Kristo amefika Kristo amefika.

152. ULIYESULUBISHWA

ULIYESULUBISHWA 1.    Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu, Uwe ngao shidani, uniombee mimi. Uliyesulubishwa, Mtakatifu Bwanangu! 2.   Wongofu sina hata, niondolee makosa. Mwovu akinishtaki nasumbuka rohoni. Wongofu sina hata, niondolee makosa. 3.   Wewe tu nipokee, nakukumbilia wee. Hata nifanye bidii, nikatoe machozi. Wewe tu nipokee, nakukimbilia wewe. 4.   Uwe ngao shidani, Niombee na mimi! Hapa nikiumizwa, Saa ya mwisho ikija: Uwe ngao shidani, Niombee na mimi!

153. NIMEPITA ULIMWENGU

NIMEPITA ULIMWENGU 1.    Nimepita ulimwengu, ulimwengu ni mzuri, lakini natamani ulimwengu mwingine. 2.    Nimeona watu wengi, hutafuta daima Maisha yao yote, ndiyo taabu na shida. 3.   Imebaki hali njema ya furaha ya roho: Hubirini popote; taabu itatulia. 4.   Msalabani pa Golgota jerahani mwa Yesu ni mahali penye raha kwao wote kabisa.

154. BARIKI YOTE YAWE MEMA

BARIKI YOTE YAWE MEMA 1.    Bariki yote yawe mema, yote yawe mbaraka. Watu wa nchi za duniani, uwajaze utukufu. Chorus: Kaa kwetu, Bwana, bariki. Uamini wee ee ndugu kweli yake Kristo. Jaa utukufu wa Bwana siku zako zote. Vaa Mwokozi ee na kweli yake, Haleluya. 2.   Nyumba za wote zibariki kwa Jina lako takata. Ujaze utukufu wako, nchi zote dunia, Kaa kwetu, Bwana… 3.   Nyosha mkono ubariki, waliojiunga nawe. Wakupokee maishani, watunzwe nawe milele. Kaa kwetu, Bwana….. 4.   Bwana yatunze mambo yote yaliyo mazuri kwako Uwape wote wakuombao, wafanikishe maisha. Kaa kwetu Bwana….

155. HAPANA RAFIKI KAMA YESU

HAPANA RAFIKI KAMA YESU 1.    Hapana rafiki kama Yesu, Yu pekee, Yu pekee; Hapana mpozi kama Yesu Yu pekee, Yu pekee. Chorus: Yesu ajua shida zetu, Aweza kutuongoza; Hapana rafiki kama Yesu, Yu pekee yu pekee. 2.   Yeye anaye sifa, ni Yesu Yu pekee, yu pekee; Ndiye aliye mnyenyekevu Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua…… 3.   Yesu pamoja nasi daima, Yu pekee, yu pekee; Kwa usiku aleta salama, Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua…… 4.   Kulinda Yesu yu Mwaminifu, Yu pekee, yu pekee; Atawakubali wahalifu, Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua….. 5.   Alipelekwa awe mwokozi, Yu pekee, yu peee; Anatutayarisha enzi Yu pekee, yu pekee; Yesu ajua…….

156. BWANA YESU YUKO WAPI

BWANA YESU YUKO WAPI 1.    Bwana Yesu yuko wapi, Mpenzi wangu rafiki? Njia gani amekwenda? Nitamwonaje mimi? Roho yangu yajutishwa Na dhambi na huzuni; Yesu mpenzi wangu Mwema Namtafuta kwa bidii. 2.    Ninapaza sauti yangu Nalia:wapi Yesu? Ndani mwangu sina raha Mpaka nimwone Yesu. Ningekuwa na mabawa Ningeruka upesi Milimani, mabondeni Kumtafuta Bwanangu. 3.   Aondoa shida zangu, Maharibifu yote. Nikiona taabu mimi Anituliza yeye. Nitafanya bidii sana; Kumtafuta popote; Sitachoka kutembea Mchana hata usiku. 4.   Bwana Yesu nitokee, Roho inakuita. Niondoe na maovu Yesu mwokozi wangu. Utilize hamu yangu Kaa kwangu daima. Nikupende sana wewe, Niwe wako milele.

157. KIJITO CHA UTAKAZO

KIJITO CHA UTAKAZO 1.    Kijito cha utakaso ni damu ya Yesu, Bwana anao uwezo kunipa wokovu. Chorus: Kijito cha utakaso, Nizame kuoshwa humo Namsifu Bwana kwa hiyo Nimepata utakaso. 2.   Viumbe vipya naona; damu ina nguvu, imeharibu uovu ulionidhulumu. 3.   Naondoka kutembea nuruni mwa mbingu, Na moyo safi kabisa kumpendeza Mungu. 4.   Ni neema ya ajabu kupakwa na damu; na Bwana Yesu kumjua Yesu wa Msalaba.

158. ANIONGOZA POPOTE

ANIONGOZA POPOTE 1.    Aniongoza popote NimwandameSiku zote Mapenzi yake ni heri Yalitimizwa kalvari. 2.    Nitaongozwa na Bwana Usiku kucha na mchana Yesu rafiki wa heri Ninakumbuka kalvari. 3.   Lanitosha neno lake Nishikwe na mkono wake Mapenzi yake ni heri Yalitimizwa kalvari. 4.   Nitaendelea mbele Pamoja naye milele Pendo lake ni hiyari Bwana Yesu wa Kalvari.

159. USHIRIKA MKUU, FURAHA YA YANGU

USHIRIKA MKUU, FURAHA YA YANGU 1.    Ushirika mkuu, furaha yangu, Kumtegemea Bwana Yesu, Nina baraka, amani pia, Kumtegemea Bwana Yesu. Chorus: Raha, Raha, Nina raha na salama, Raha, Raha, kwa kumtegemea Yesu. 2.   Ni halisi kutembea naye, Kwa kumtegemea Yesu. Naona nuru njiani mwangu, Kumtegemea Bwana Yesu. 3.   Sioni shaka wala hasara, Kumtegemea Bwana Yesu; Nina amanikwake Mwolozi, Kumtegemea Bwana Yesu.

160. JIONI MOYO WANGU

JIONI MOYO WANGU 1.   Jioni moyo wangu wakutafuta Bwana, na kukushukuru. Unikazie macho yenye baraka nyingi, ung’aze mwili na roho. 2.   Natumaini tena rehema yako Baba hata usiku huu. Fukuza majaribu na hila ya shetani, ukiwa karibu yangu. 3.   Unanipenda sana, wakaa pamoja nami, wanikaribisha. Unanifurahisha kwa wema wako mwingi, sababu hii nakusifu. 4.   Maisha yanapita upesi, ni safari ya kwenda mbinguni. Unifundishe, Bwana, kuelekea kwako: Pazuri ni mbinguni tu.

161. USIKU UINGIAPO

USIKU UINGIAPO 1.   Usiku uingiapo, umwaze Mungu Mkuu, aendeshaye dunia kwa mwendo mtulivu. 2.   Kwa nini wahangaika usiku namchana? Umtwishe huzuni yako aliyekuumba. 3.   Kwake haujapunguka uwezo na msaada. Atayatimiza yote aliyoyaanza. 4.   Ukamwachie kutenda atakalo kwako! Kwa hiyo ulale raha na kufurahiwa.