155. HAPANA RAFIKI KAMA YESU

HAPANA RAFIKI KAMA YESU

1.  Hapana rafiki kama Yesu,
Yu pekee, Yu pekee;
Hapana mpozi kama Yesu
Yu pekee, Yu pekee.

Chorus:
Yesu ajua shida zetu,
Aweza kutuongoza;
Hapana rafiki kama Yesu,
Yu pekee yu pekee.

2.  Yeye anaye sifa, ni Yesu
Yu pekee, yu pekee;
Ndiye aliye mnyenyekevu
Yu pekee, yu pekee;
Yesu ajua……

3.  Yesu pamoja nasi daima,
Yu pekee, yu pekee;
Kwa usiku aleta salama,
Yu pekee, yu pekee;
Yesu ajua……

4.  Kulinda Yesu yu Mwaminifu,
Yu pekee, yu pekee;
Atawakubali wahalifu,
Yu pekee, yu pekee;
Yesu ajua…..

5.  Alipelekwa awe mwokozi,
Yu pekee, yu peee;
Anatutayarisha enzi
Yu pekee, yu pekee;
Yesu ajua…….

Comments

Popular posts from this blog

140. MAHALI NI PAZURI

144. MBELE NINAENDELEA

141. PANA JITO, LINA MAJI MAZURI