147. TEGEMEA HADI KUFA
TEGEMEA HADI KUFA
1. Tegemea mpaka kufa,
Utapata wokovu.
Bwana Yesu ni Mwokozi
Yeye anakupenda.
Uje kwake ‘sikawie’.
Yeye akuokoa.
Chorus:
Njoo upesi! Njoo upesi!
Fika kwa Bwana Yesu.
2. Acha mambo ya dunia
Yakuhangaishayo.
Iko mali ya uzima
Unaitiwaa hiyo.
Mali hiyo ni uzima
Utapewa na Bwana.
Njoo upesi! …
3. Wakatae, waepuke
Wanaokudanganya;
Na wajinga, wakuponza,
Wakupoteza wewe.
Ila wewe ukatae
Kuondoka kwa Yesu.
Njoo upesi! …
4. Ukijua jambo hilo
Usipolifuata
Kosa hilo kubwa sana,
Wapasiwa hukumu.
Vumilia, jizuie
Utapata uzima.
Njoo upesi! …
5. Bwana Yesu amekwisha
Kukutengenezea
Kitu chema kwake Mungu,
Ndiko unakokwenda.
Kile kitu upendacho
Kule utakipewa.
Njoo upesi! …
Comments
Post a Comment