157. KIJITO CHA UTAKAZO

KIJITO CHA UTAKAZO

1.  Kijito cha utakaso
ni damu ya Yesu,
Bwana anao uwezo
kunipa wokovu.

Chorus:
Kijito cha utakaso,
Nizame kuoshwa humo
Namsifu Bwana kwa hiyo
Nimepata utakaso.

2.  Viumbe vipya naona;
damu ina nguvu,
imeharibu uovu
ulionidhulumu.

3.  Naondoka kutembea
nuruni mwa mbingu,
Na moyo safi kabisa
kumpendeza Mungu.

4.  Ni neema ya ajabu
kupakwa na damu;
na Bwana Yesu kumjua
Yesu wa Msalaba.

Comments

Popular posts from this blog

140. MAHALI NI PAZURI

144. MBELE NINAENDELEA

141. PANA JITO, LINA MAJI MAZURI