137. YESU MPONYA
YESU MPONYA
1. Yesu ndiye mganga wetu
Aponya wagonjwa wote;
Mganga wetu ni Yesu,
Aponyaye hasira.
Chorus:
Tumsifu huyo Yesu
Tumsifu milele,
Kwani Mponya mtakata
Mwokozi wa wanyonge.
2. Mganga wetu ni Yesu
Huondoa matusi;
Mganga wetu ni Yesu,
Mwenye kuponya choyo.
3. Mganga wetu ni Yesu
Huponya wivu wetu;
Yesu ndiye aponyae
Kelele za nyumbani.
4. Mganga wetu ni Yesu
Mponya wa tamaa mbaya;
Mganga wetu ni Yesu
Uasherati hufuta.
5. Mganga wetu ni Yesu
Aponya kiu cha pombe,
Mganga wetu ni Yesu
Kila dhambi uponya.
Comments
Post a Comment